UBIDIFU WA MLINDA LANGO VICTOR ODHIAMBO WAHITAJIKA ZAIDI

city Stars celebrate the equalizer

Mlinda lango wa klabu cha City Stars Victor Odhiambo ana kibarua kigumu cha  kukipa klabu chake huduma ya kujituma zaidi .

Odhiambo ndiye tegemeo katika klabu hicho kama mlinda lango na hana budi kuongeza makali yake ili kuokoa klabu hicho kilicho na ngome thabiti mtaani kawangware .

Klabu hicho kitacheza ngoma dhidi ya Sofapaka leo alasiri katika ugha wa kaunti ya machakos.

Advertisements

CAROLYNE ODHIAMBO APIGWA DHAFRAU LA FAINI

Court

Football Kenya Limited ,FKF imempa kadi nyekundu mchezaji wa klabu cha Green Berrets Carolyne Odhiambo baada ya mchezaji huyo kumpiga muamuzi katika mechi yao dhidi ya Kangemi All Stars .

Mechi hiyo iliyosakatwa Kwenye ugha wa Kabete Technical mnamo july tarehe 11 ,ilikatizwa ghafla baada ya vugu vugu huo .

Katika waraka ulioandikwa na msimamizi wa FKF bwana Samson Cherop,mchezaji huyo hatoshiriki  katika mchuano wowote hadi msimu ujao  na kupigwa faini isiyojulikana.

WAAMUZI WATEULIWA NA FIFA

whistle

Waamuzi wa mechi ya  kufuzu ya olimpiki  upande wa akina dada  ,Harambee starlets dhidi ya Banyana Banyana itakayogharagazwa ughani machakos wameteuliwa.

Muamuzi wa kati ni Bedoui Ghabi mwasili wa Tunisia akipokea nguvu kazi kutoka kwa Haced Amel na Hendaoui Chefia.

Msimamizi wa nne ni Abdelaoued Lilia na kamishna Isabella Kapera kutoka Tanzania.

Mechi hiyo itasakatwa jumapili ijaayo.

OKUMBI AELEKEZA KIDOLE CHA LAWAMA KWA MUAMUZI

Mathare United team

Mkufunzi mkuu wa klabu cha Mathare Stanley Okumbi amemlaumu muamuzi wa mechi yao dhidi ya KCB iliyoisha sare 2-2.

Okumbi amedai  kuwa muamuzi huyo alitumia mamlaka ya kupuliza kipenga visivyo  huku akiwapendelea wapinzani wao.

Alisema kuwa hawaku histahili sare kwa kuwa klabu chake kilicheza mechi ya kutia ladha walakin hawakupiku kwa sababu ya maamuzi tasa ya muamuzi.

Aliomba wasimamizi wa KPL kuwateua waamuzi waliobobea kwa mechi kubwa zanazo histahili umaarufu,usawa na haki .

Klabu hicho sasa kimekita hema nafasi ya tisa kwenye jedwali ya ligi  kwa alama 26

MAWASILIANO HAFIFU YAMZINGUA LOGARUSIC

Zdravko Logarusic

Mkufunzi wa klabu cha AFC  Leopards  Zdrako Logarusic amesema kuwa hajapata mawasiano yoyote kutoka  kwa wasimamizi wa klabu hicho huku hali ya vuta ni kuvute dhidi yake na wasimamizi ikishuhudiwa.

Mkufunzi huyo alisusia kusafiri na klabu hicho   mjini Awendo kwa mechi ya mchuano wa KPL dhidi ya Sony Sugar.

Kocha huyo amegadhabishwa na hali ya kutojali ya wasimamizi kuhusu marupurupu yake huku akiwalaani wengine kwa kumtumia arafa ya chuki mbadala na kutafuta suluhu thabiti.

Akihutubia wanahabari,Logarusic amesema kuwa hakuna hata mmoja aliyemjulia hali kama yu hai tangu mechi yao kati ya  City Stars wiki iliyopita.

Klabu hicho kinatarajiwa kusakata dimba dhidi ya Sony bila mkufunzi huyo.

LOGARUSIC: HUDUMA NI BAADA YA MALIPO

Logarusic now an AFC

mkufunzi wa klabu cha AFC Leopards  Zdravko Logarusic amesusia kusafiri na timu yake mjini Awendo kusakata mechi dhidi ya Sony sugar kwa madai ya kutolipwa na klabu hicho.

Nduru za kuaminika za tuarifu kuwa kocha huyo  hajafika uwanjani tangu wikendi iliyopita walipogaragaza mechi dhidi ya City Stars .

Timu hiyo inaendelea kunawia kwenye bahari ya ufukara ,dhidi na jakamoyo kwa ukosefu wa mfadhili huku mchango wa kihela ikipangwa kufanyika hivi karibuni katika hoteli ya pan afric.

Wandani wa klabu hicho wanasema kuwa harakati kabambe imeandaliwa kumrudisha mkufunzi huyo uwanjani huku kocha huyo akishikilia kutorudi hadi kulipwa .

Msimu huu umekuwa mgumu zaidi kwa vilabu wembe nchini  ,ikiwemo kiranja Gor mahia baada ya kubwagwa na wafadhili wa msimu uliopita.

MSURURU WA FKF

NO Team M PT
1 Kakamega Homeboyz 19 41
2 Posta Rangers 18 34
3 Zoo Kericho 17 34
4 Kariobangi Sharks 18 33
5 Nzoia United 17 31
6 Shabana 17 29
7 Bidco United 18 28
8 West Kenya Sugar 18 26
9 Nakumatt 17 24
10 Oserian 18 22
11 Ligi Ndogo 17 20
12 Agrochemicals 18 20
13 Nairobi Stima 18 18
14 Finlays Horticulture 17 15
15 Modern Coast Rangers 18 15
16 MOSCA FC 19 15
17 St Joseph FC 18 14
18 FC Talanta 18 13

Kakamega homeboyz wanaendelea kunawiri kwenye bahari ya dimba  kwa pointi 41 huku FC Talanta wadidimia kwa pointi 13.

MSURURU WA KPL

# Team M W D L GF GA GD PT
1 Gor Mahia 18 14 4 0 37 8 29 46
2 Ulinzi Stars 19 11 4 4 27 16 11 37
3 Tusker FC 20 10 5 5 38 18 20 35
4 AFC Leopards 19 10 4 5 25 15 10 34
5 Sofapaka 19 9 6 4 24 23 1 33
6 Bandari 19 8 5 6 19 15 4 29
7 Western Stima 20 8 5 7 19 17 2 29
8 Ushuru FC 20 7 6 7 16 17 -1 27
9 Mathare United 19 5 10 4 24 19 5 25
10 Thika United 20 7 4 9 19 28 -9 25
11 Muhoroni Youth fc 19 4 8 7 16 27 -11 20
12 Chemelil Sugar 19 3 9 7 14 25 -11 18
13 KCB 19 4 4 11 21 27 -6 16
14 SoNy Sugar 18 4 4 10 10 18 -8 16
15 Nairobi City Stars 19 2 7 10 13 24 -11 13
16 Nakuru AllStars 19 1 7 11 16 41 -25

TTT